1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu wahamishwa kufuatia mafuriko Ujerumani

3 Juni 2024

Maelfu ya watu wamehamishwa kutoka makaazi yao kusini mwa Ujerumani kufuatia mafuriko yaliyosababisha kifo cha afisa mmoja wa uokoaji na angalau mtu mmoja kutojulikana alipo.

https://p.dw.com/p/4gYf7
Jimbo la Baden-Württemberg - Meckenbeuren lilivyofurika
Jimbo la Baden-Württemberg lilivyofurikaPicha: Felix Kästle/dpa

Watu wameokolewa katika vijiji kadhaa vilivyoko pembezoni mwa mto Danube na Schmutter huku afisa mmoja akielezea wasiwasi kuhusiana na kufurika kwa bwawa lililoko eneo hilo.

Ujerumani Mafuriko Bayern - Wertingen
Maafisa wa uokoaji wakiwaokoa watu kwa mtumbwiPicha: Stefan Puchner/dpa/picture alliance

Kulingana na idara ya hali ya hewa ya Ujerumani, mvua kubwa na mafuriko iliyoshuhudiwa katika majimbo mawili imetatiza shughuli za kawaida kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita na mvua nyingi zaidi inatarajiwa kunyesha.

Jumla ya waokoaji wa dharura 40,000 wameshiriki juhudi hizo za uokoaji tangu Ijumaa. Jeshi la Ujerumani pia limelazimika kuingilia kati juhudi hizo wakati ambapo mito katika jimbo hilo la Bavaria ikiwa inazidi kufurika.