1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Nigeria atangaza punguzo la bei ya mafuta ya petroli

16 Januari 2012

Rais Jonathan ametangaza punguzo la bei ya petroli kwa asilimia 30 katika juhudi za kumaliza mgomo ambao unaingia wiki ya pili, huku wanajeshi wakichukua udhibiti wa eneo kuu linalofanyiwa maandamano mjini Lagos.

https://p.dw.com/p/13kAT
Demonstrators protest against the elimination of a popular fuel subsidy that has doubled the price of petrol in Nigeria's captial Abuja, January 10, 2012. Nigerians took to the streets on Tuesday in growing numbers on the second day of protests against a sharp increase in petrol prices, piling pressure on President Goodluck Jonathan to reverse his removal of fuel subsidies. REUTERS/Afolabi Sotunde (NIGERIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST ENERGY)
Wananchi wa Nigeria wakiandamana kutokana na ughali wa petroli.Picha: dapd

Rais Jonathan ametangaza hatua hiyo katika hotuba yake kwa taifa kwa njia ya televisheni baada ya wiki ambayo amekuwa kimya , wakati mgomo na maandamano ya umma yakizuwia shughuli muhimu katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya wakaazi katika bara la Afrika , ambayo ni mtoaji mkubwa wa mafuta katika bara hilo.

Rais amedai kuwa maandamano yametekwa nyara na watu ambao amewaeleza kuwa wanataka kuchochea hali ya kutokuelewana , unaharibifu na hali ya kutokuwa na usalama . Rais Jonathan hakutoa maelezo zaidi katika madai yake hayo , lakini hotuba yake inaonyesha ni jinsi gani serikali yake imekuwa na wasi wasi kutokana na maandamano yanayoikumba nchi hiyo.

epa03046191 (FILE) A file photograph Goodluck Ebele Jonathan, President and Commander-in-Chief of the Armed Forces of the Federal Republic of Nigeria speaks during the general debate at the 66th session of the United Nations General Assembly at United Nations headquarters in New York, New York, USA, on 21 September 2011. Media reports state on 31 December 2011 that President Goodluck Jonathan has declared a state of emergency in areas affected by attacks from the Islamist group Boko Haram. Borders will be temporarily closed in the north-eastern states of Yobe and Borno, and central state of Plateau. EPA/JASON SZENES *** Local Caption *** 00000402928322 +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais Goodluck Jonathan wa NigeriaPicha: picture-alliance/dpa

Rais Goodluck Jonathan katika hotuba yake leo asubuhi amesema kuwa serikali itatoa ruzuku kwa bei ya petroli ili kupunguza haraka bei ya mafuta hadi kiasi cha dola 2.75 kwa galoni huku kukiwa na mgomo wa nchi nzima ambao umeathiri taifa hilo la Afrika magharibi.

Serikali itaendelea na hatua yake ya kuibinafsisha sekta ya mafuta. Hata hivyo kutokana na matatizo yaliyowakabili Wanigeria , na baada ya kutafakari na kujadiliana na magavana wa majimbo na uongozi wa bunge , serikali imeidhinisha upunguzaji wa bei ya mafuta hadi naira 97 kwa lita.

A cabbage cleaner stands in front of fuel trucks in Lagos, Nigeria, Sunday, Jan. 15, 2012. Nigeria's government and labor unions failed to end a paralyzing nationwide strike over the high costs of gasoline, and potentially sparking a national oil production shutdown. (Foto:Sunday Alamba/AP/dapd)
Mgomo dhidi ya kupanda kwa bei ya petroliPicha: dapd

Hotuba ya Jonathan inakuja baada ya jaribio lake la kufanya majadiliano na vyama vya wafanyakazi kushindwa jana jumapili kumaliza mgomo ambao unaingia siku yake ya sita leo. Rais wa chama kikuu cha wafanyakazi nchini Nigeria Abdulwaheed Omar amesema mapema leo Jumatatu kuwa amesitisha kwa muda maandamano yaliyopangwa kufanyika leo Jumatatu baada ya rais Jonathan kutangaza punguzo hilo la bei ya mafuta .

Mgomo ulianza Januari 9 na kusababisha shughuli kusita katika taifa hilo lenye wakaazi wanaofikia milioni 160.

Mzizi wa fitina unabaki kuwa bei ya mafuta. Serikali ya Goodluck Jonathan iliondoa ruzuku katika bei ya mafuta , ruzuku ambayo inaweka bei ya mafuta kuwa chini.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / ape

Mhariri : Mohammed Khelef