Rais Kikwete ziarani nchini Marekani
20 Mei 2009Matangazo
Tanzania ni mshirika imara wa Marekani katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara na itakuwa ziara ya kwanza ya kiongozi wa kiafrika katika Ikulu ya Marekani tangu Obama ashike rasmi wadhifa wa Urais Januari mwaka huu.
Mohamed Abdulrahman alizungumza na Profesa Frank Chiteji akiwa Marekani na kwanza alimuuliza ziara hii ina umuhimu gani na anafikiri ni masuala gani yatakayopewa kipa umbele.
Mwandishi: Mohamed Abdulrahman
Mhariri: Thelma Mwadzaya