Rais Hamid Karzai aongoza kwa mara ya pili | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 17.09.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Rais Hamid Karzai aongoza kwa mara ya pili

Ujerumani imesisitiza kuwa matokeo ya uchaguzi wa rais ya Afghanistan ni ya muda mpaka pale madai ya hila na udanganyifu yatakapochunguzwa kikamilifu.

default

Waangalizi wa Uchaguzi wa EU,Afghanistan

Kulingana na waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya walioko nchini Afghanistan kiasi cha kura milioni 1.5 huenda zilikuwa na hila.

Kulingana na matokeo ya muda yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Afghanistan baada ya kuzihesabu upya baadhi ya kura zilizopigwa Rais Hamid Karzai amepata takriban asilimia 55 ya kura zote.Mpinzani wake mkuu Abdullah Abdullah anaripotiwa kuwa amepata kiasi cha asilimia 28 ya kura zote.Hali hiyo imeifanya Tume ya Uchaguzi inayohusika na matatizo ya uchaguzi imeamrisha kiasi cha asilimia 10 ya kura zote kuhesabiwa upya.

Thelma Mwadzaya/ AFPE,DPAE

 • Tarehe 17.09.2009
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/JiWA
 • Tarehe 17.09.2009
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/JiWA

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com