Rais Ahmadinejad aionya Israel dhidi ya kuivamia Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 18.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais Ahmadinejad aionya Israel dhidi ya kuivamia Iran

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad ametoa kauli kali kufuatia jaribo la kombora la Israel hapo jana.

Katika mahojiano yake na televisheni ya Al Jazeera, kiongozi huyo amesema Israel haitajaribu kuivamiawa jamhuri ya kiislamu ya Iran.

Aidha kiongozi huyo amesema iwapo Israel itaishambulia Iran serikali ya mjini Tehran itaishambulia Israel.

Rais Ahmadinejad pia ametoa matamshi makali kwa rais wa Marekani, George W Bush, akimshutumu kiongozi huyo kwa kueneza ujumbe wa malumbano wakai wa ziara yake ya Mashariki ya Kati.

Rais Bush alitumia muda mwingi wakati wa ziara yake akitafuta kuungwa mkono na nchi za kiarabu kuhusu msimamo mkali dhidi ya Iran.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com