1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PORT ARHUR : Kimbunga Rita changuruma Marekani

24 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEYC

Kimbunga Rita kinanguruma katikka mwambao wa Marekani kikiandamana na upepo unaokimbia kwa kilomita 205 kwa saa na kusababisha vifo pamoja na mafuriko mapya kwa mji wa New Orleans ambao tayari umeharibiwa na kimbunga cha Katrina kilichopiga awali.

Zaidi ya watu milioni mbili na nusu wameukimbia ukanda wa mwambao wa kilomita 500 kuanzia Port O’Conor huko Texas hadi New Orleans huko Loussiana lakini inaonekana kimbunga hicho kinaelekea eneo la Port Arthur lililosheni vituo vya kusafishia mafuta na viwanda vya kemikali.

Uzalishaji wa asilimia 99 ya mafuta nchini Marekani na asilimia 72 ya gesi asili katika Ghuba ya Mexico tayari umesitishwa wakati makampuni yakitelekeza vituo vyao vya uzalishaji mafuta.

Wakati kimbunga hicho cha Rita kikaribia tayari kimevunja maboma ya kuzuwiya maji ya bahari katika maeneo ya pwani ya mji wa New Orleans.Mapema basi lililokuwa limewachukuwa wazee waliokuwa wakikimbia kimbunga hicho limewaka moto karibu na mji wa Dallas katika jimbo la Texas na kuuwa abiria 24.

Ingawa kasi ya kimbunga hicho imepunguwa lakini bado kinategemewa kuwa cha hatari wakati kitakapopiga leo hii na watu wamekuwa wakiendelea kujaa kwenye mabasi,magari,ndege za binafsi na wengine wakiwa kwenye baiskeli wakiikimbia miji ya mwambao.