1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Ufilipino na Marekani kuanza luteka ya pamoja ya kijeshi

22 Aprili 2024

Maelfu ya wanajeshi wa Ufilipino na Marekani wataanza hii leo luteka ya pamoja ya kijeshi, huku ushawishi na nguvu za China vikiongezeka katika eneo hilo na kuzua hofu ya kutokea mzozo.

https://p.dw.com/p/4f28A
Marekani | Rais Biden akiwapokea Fumio Kishida na Ferdinand Marcos Jr.
Rais wa Marekani Joe Biden(katikati) akiwa na Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr. (kushoto) pamoja na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida mjini WashingtonPicha: Kevin Lamarque/REUTERS

Mazoezi hayo ya kila mwaka yaliyopewa jina la Balikatan au "bega kwa bega", yatafanyika katika maeneo ya kaskazini na magharibi mwa taifa hilo la visiwa, karibu na maeneo ya Kusini mwa Bahari ya China na Taiwan.   

China inadai umiliki wa karibu ukanda mzima wa baharini, ambao ni njia muhimu ya biashara ya kimataifa na pia inaichukulia Taiwan kuwa sehemu ya eneo lake. Katika kukabiliana na ongezeko la ushawishi wa China, Marekani imekuwa ikiimarisha ushirikiano na nchi za  eneo la Asia na Pasifiki ikiwemo Ufilipino.

China imesema hii leo kuwa ipo tayari kusuluhisha mizozo ya baharini na nchi zingine kupitia njia ya mazungumzo lakini haitajiruhusu "kunyanyaswa", huku ikitoa wito wa kutegeuza Bahari kuwa eneo la kutunishiana misuli.