1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa afikisha ujumbe wa amani na mshikamano Algeria

Amina Abubakar afp,reuters,dpa
13 Aprili 2026

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV, anaendelea na ziara yake Algeria, alikowasili huko akitoa wito kwa ajili ya amani na kukomeshwa tabia za ukoloni mamboleo katika masuala ya kidunia.

https://p.dw.com/p/5C6mb
Algerien Algier 2026 | Papst Leo XIV. besucht das Märtyrer-Denkmal Maqam Echahid
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIVPicha: Guglielmo Mangiapane/REUTERS

Uwepo wa Papa Leo mjini Algiers, Algeria  ndio mwanzo wa ziara yake ya siku 11 itakayomfikisha katika mataifa mengine matatu ya Bara la Afrika ikiwa ni pamoja na Cameroon, Angola na Equatorial Guinea. Papa ameingia kwenye historia ya kuwa kiongozi wa kwanza mkuu wa kikatoliki kufanya ziara iyo kubwa barani Afrika.

Kiongozi huyo wa kiroho yupo Algeria na ujumbe wa kuishi pamoja na kuvumiliana kati ya mataifa yaliyo na waislamu na wakristo walio wengi, hasa katika kipindi hiki cha migogoro na pia kumuenzi mtakatifu Agostino aliyechangia safari ya kidini ya Papa Leo.

Trump amkosoa Papa hadharani

Lakini ziara hiyo ilianza kwa maneno makali kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Papa huyo, aliyezaliwa katika  jimbo la Chicago, Marekani. Trump alianza kwa kumwambia Papa aache kuukingia kifua utawala ulio na itikadi kali na unaotaka kumiliki silaha za nyuklia, akisema Papa ni dhaifu na ni mtu asiyejiamini kuhusu kusitisha uhalifu.

USA Washington D.C. 2026 | Donald Trump verlässt das Weiße Haus
Rais wa Marekani Donald Trump Picha: Annabelle Gordon/REUTERS

Papa nae akajibu vikali kauli hiyo akisema amani na maridhiano ni mambo yanayohimizwa katika injili, akisisitiza kwamba injili haihubiri vita na kamwe hauogopi utawala wa rais Trump na wala hana hofu ya kusema kile Injili inalohimiza. Trump amekuwa akimkosoa Papa kwa kutoa wito wa kumalizika kwa mgogoro wa Mashariki ya Kati. 

Papa leo aomba amani itawale dunia

Baada ya Papa kuwasili Algiers pia alisisitiza uwepo uo huo wa amani kwa walgeria, walipigania uhuru kutoka kwa Ufaransa, uliopatikana mwaka 1962.Maelfu kwa maelfu waliuwawa wakati huo, wakati vikosi vya ufaransa vilivyowatesa wafungwa na wengine kupotea kama sehemu ya kutaka kuendelea kuliongoza taifa hilo.

Algerien Algier 2026 | Papst Leo XIV. hält Rede am Märtyrer-Denkmal Maqam Echahid
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV yupo Algeria katika kituo chake cha kwanza cha ziara ya siku 11 barani Afrika,Picha: Guglielmo Mangiapane/REUTERS

Baadae Papa atakutana na rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune pamoja na viongozi wengine. Papa aliwapongeza raia wa taifa hilo kwa heshima na umoja walionao, akisema hilo ndilo linalohitajika kwa sasa kuliko wakati mwengine wowote hasa wakati dunia ikiandamwa na matukio ya ukiukwaji wa sheria za kimataifa na tabia za ukoloni mambo leo.

Papa Leo hakutoa mifano lakini amekuwa akizungumzia kwa uwazi vita vya Urusi na Ukraine, vita vya Iran na hata uvamizi wa Israel Kusini mwa Lebanon.

Wasiwasi Camroon kuelekea ziara ya Papa

Huku hayo yakiarifiwa kuna minon'gono yanayoendelea nchini Cameroon ambayo ndio nchi ya pili papa atakayoitembelea ikiwa ni sehemu ya ziara yake barani Afrika.

Kamerun Yaoundé 2025 | Präsident Paul Biya gibt Stimme bei Präsidentschaftswahl ab
Rais wa Cameroon Paul Biya Picha: Zohra Bensemra/REUTERS

Wakatoliki wa taifa hilo wanadai kuwa huenda ziara hiyo ikammpa nafasi Rais wa miaka mingi Paul Biya, kusafisha jina lake  ikiwa ni miezi sita baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliokuwa na utata.

Papa Leo atakutana na Biya siku ya Jumatano na tayari picha zinazomuonesha Papa akiwa amesimama karibu na rais Biya aliye na miaka 93, zimebandikwa kote mjini Yaounde.