OUGADOUGOU: Filamu ya Maseko yatunukiwa zawadi | Habari za Ulimwengu | DW | 06.03.2005
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

OUGADOUGOU: Filamu ya Maseko yatunukiwa zawadi

Mwongozaji wa filamu Zola Maseko ni mwananchi wa kwanza wa Afrika Kusini kushinda zawadi kuu katika Sherehe ya Filamu barani Afrika iliyofanywa Burkina Faso.Filamu yake iitawyo "Drum" iliyoshinda zawadi ya kwanza ni hadithi inayohusika na ubaguzi wa rangi katika vilabu vya jazz katika miaka ya hamsini mjini Johannesburg.Maseko ametunukiwa Sanamu ya Yennenga na zawadi ya Dola 20,000.Filamu nyingine ya Afrika Kusini "U-Carmen eKhayelitsha" mwezi wa Februari ilishinda zawadi katika Sherehe ya Filamu,mjini Berlin.