1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Berlinale

Likifahamika pia kama Tamasha la Kimataifa la Filamu la Berline, Berlinale ndiyo tukio muhimu zaidi la filamu la Ujerumani na linahudhuriwa na maelfu ya wadau wa sekta hiyo na watu mashuhuri kila mwaka.

Tamasha la Berlinale linafanyika katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin Februari kila mwaka, likionyesha filamu zipatazo 400 za Kijerumani na kimataifa na kuhudhuriwa na wageni karibu 500,000. Lilianzishwa 1951 na limekuwa tamasha kuu la filamu la Ujeurmani. Tamasha hilo la siku 10 ambalo limeongozwa na Dieter Kosslick tangu 200, linahitimishwa kwa kutolewa tuzo za dubu za dhahabu na fedha.