Olmert akutana na Merkel mjini Berlin | Habari za Ulimwengu | DW | 12.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Olmert akutana na Merkel mjini Berlin

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert mjini Berlin hii leo kujadili maswala kama vile mzozo wa eneo la Ukanda wa Gaza na mpango wa nyuklia wa Iran.

Olmert, ambaye yuko katika zaira ya siku tatu hapa Ujerumani, amesisitiza atazilinda jamii za wayahudi zinazolengwa na mashambulio ya maroketi ya wapalestina yanayovurumishwa kutoka Ukanda wa Gaza.

Kansela Angela Merkel na waziri mkuu Ehud Olmert wanapanga kufanya mazungumzo zaidi kabla kiongozi wa Israel kurudi nyumbani baadaye leo.

Maafisa wa Israel wanasema katika mazungumzo yake na kansela Merkel, waziri mkuu Olmert atataka shinikizo zaidi la kimataifa dhidi ya Iran katika Umoja wa Mataifa, ambako azimio la vikwazo vipya limetayarishwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com