Asilimia 52 ya Waingereza wamepiga kura kusema wanataka nchi yao ijitoe kwenye Umoja wa Ulaya. Kura hiyo ya maoni imetikisa siasa za Uingereza na kumfanya Waziri Mkuu David Cameron kutangaza nia ya kujiuzulu. Katika kipindi cha Maoni, Mohammed Khelef na wachambuzi wanajadili hatma ya Uingereza.