Ni miaka 60 tangu siku ya wakimbizi duniani kuasisiwa | Habari za Ulimwengu | DW | 20.06.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ni miaka 60 tangu siku ya wakimbizi duniani kuasisiwa

Kwa mujibu wa Shirika linalohudumia wakimbizi duniani, UNHCR jumla ya wakimbizi, wanaotafuta hifadhi, na wakimbizi wa ndani inazidi kuongezeka hadi kukaribia watu milioni 44, kwa mwaka 2010.

default

Antonio Guterres,Kamishna wa Shirika la UNHCR la Wakimbizi

Umoja wa Mataifa umechukua hatua ya kusahihisha kile kilichoitwa "shaka isiyo sahihi" kuhusu mtawanyiko wa watu katika maeneo tofauti  kwa kusema kwamba nchi zinazoendelea zina kiasi ya asilimia 80 ya wakimbizi wote wa Duniani.

Kamishna wa Umoja wa Mataifa  anaeshughulikia suala la wakimbizi , Anthonio Gutterres amesema hivi sasa kumekuwa na mashaka kuhusu mwenendo wa wakimbizi na vielelezo vya jitihada za kimataifa za kudhibiti hali hiyo.

Lybien Choucha Flüchtlinge Flash-Galerie

Wakimbizi wa Libya kwenye kambi ya Choucha iliyoko Tunisia

Amesema hofu ya kwamba nchi zilizoendelelea zina idadi kubwa ya wakambizi inatokea kwa makosa na hasa kutokana na kuchanganywa na suala la uhamiaji haramu.

Kamishina huyo wa UNHCR, anaehudumia wakimbizi amesema nchi masikini bado zinabeba mzigo mzito wa wakimbizi.

Ripoti ya mwaka ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNCR inaonesha kuwa, nchi zinazoendelea, zikiwemo ambazo masikini kupita kiasi ndizo zilizoathirika zaidi kwa kuwa na wakimbizi wengi.

Refugees.jpg

Wakimbizi: UNHCR yasema nchi masikini zinabeba mzigo mkubwa

Pakistan inaongoza kwa kuwa na wakimbizi milioni 9.1, Iran ina wakimbizi milioni 1.1 na Syria ikiwa na wakimbizi milioni.

Gharama pia za kuhudumia wakimbizi hao zimekuwa kubwa, nchi za Pakistan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Kenya zinaatrhirika kwa kiasi kikubwa katika pato lake la jumla taifa kwa kufanikisha huduma mbalimbali za wakimbizi hao ikilinganishwa na nchi kama Ujerumani.

Kwa ujumla hivi sasa kuna jumla ya kiasi ya watu milioni 43.7 waliyoyakimbia makazi yao duniani kote, ikijumuisha wakimbizi milioni 15.6. Kiasi cha watu milioni 27.5 ni wakimbizi wa ndani.

Takwimu hizo za mwaka uliyopita zinaonesha pia kuna idadi nyingine ya watu 850,000 wanaotafuta hifadhi.

Ripoti hiyo iliyotolewa katika hafla ya kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani inaonesha kuwa, kiwango kilichoainisha kuwa cha juu kufikiwa kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita.

Afghanstan inaonesha idadi kubwa ya wakimbizi ya kiasi ya milioni tatu, ikifuatiwa na Iraq yenye wakimibizi milioni 1.6, Somalia 770,200, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo 476,000 na Myamar wakimbizi 415,700.

UNHCR Botschafterin Angelina Jolie in Bosnien und Herzegowina Flash-Galerie

Balozi wa Nia Njema wa UNHCR Angelina Jolie akiwa Bosnia.

Nchi ambayo imekuwa chaguo la wengi la watu wanaoomba hifadhi ni, Afrika ya Kusini iliyopokea maombi 180,600 kwa mwaka 2010 ikiwa ni mara tatu ya Marekani yenye maombi 54,300 au Ufaransa yenye maombi 48,100.

Lakini takwimu hizi hazijumuishi hali ya mambo iliyopo sasa na hasa baada ya kuzuka mizozo katika nchi za Libya, Cote d'Ivoire na Syria.

Kutokana na hali ya vuguvugu la kisiasa huko maeneo ya Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati ,  nchi za ulaya zimekuwa na shaka kubwa ya ongezeko la wimbi la waakimbizi kwa sasa.

Mwandishi: Sudi Mnette//AFP

Mhariri:Yusuf Saumu

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com