NEW DELHI: Watu 64 wauwawa kwenye shambulio dhidi ya treni | Habari za Ulimwengu | DW | 19.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW DELHI: Watu 64 wauwawa kwenye shambulio dhidi ya treni

Watu takriban 64 wameuwawa wakati treni walimokuwa wakisafiria ilipowaka moto mapema leo kaskazini mwa India.

Kwa mujibu wa afisa wa usafiri wa reli katika eneo hilo, moto huo huenda ulisababishwa na bomu. Kifaa cha kuripuka kimepatikana karibu na reli ambapo treni hiyo ilianza kuwaka moto.

Moto huo umeyaharibu mabehewa mawili ya treni hiyo, mojawapo ya treni mbili zinazoiunganisha India na Pakistan. Treni hiyo ilikuwa njiani kutoka mjini New Delhi India ikielekea mji wa Atari, kituo cha mwisho cha treni kabla kufika mpaka wa Pakistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com