NAIROBI:Maporomoko ya ardhi yaua watu 18 | Habari za Ulimwengu | DW | 12.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI:Maporomoko ya ardhi yaua watu 18

Takriban watu 18 wameuwawa kufatia maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku jana kaskazini mwa mji wa Kakamega magharibi mwa Kenya.

Watu wengine wapatao 56 wamejruhiwa katika mkasa huo uliotokea katika kijiji cha Kuvasali kinachopakana na kaskazini mwa Nandi.

Miongoni mwa waliouwawa ni mwanamume mmoja na familia yake akiwemo mkewe na mtoto wao wa kike ambao walifunikwa na tope ndani ya nyumba yao walikuwa wamelala.

Inahofiwa huenda idadi ya watu waliokufa ikaongezeka, kwa mujibu wa mkuu wa wilaya bwana Kenedy Nyaiyo.

Kijiji cha Kuvasali kiko katika kata ya Ikoli eneo bunge la Malava kilomita 50 kutoka Mji wa Kakamega.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com