Mwaka mmoja baada ya kurejea kwa demokrasia nchini Pakistan | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.02.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mwaka mmoja baada ya kurejea kwa demokrasia nchini Pakistan

tathmini ya mwaka mmoja wa demokrasia nchini Pakistan inaonyesha wazi kuwa hali bado si shwari. Hususan hali ya usalama katika maeneo ya mpaka na afghanistan, ambayo imezidi kuwa mbaya.

default

Rais wa Pakistan , ambaye ni mume wa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, aliyeuwawa Benazir Bhutto, Asif Zardari , wakati akitoa hotuba yake bungeni Septemba 20 mwaka jana.


Uchaguzi wa bunge nchini Pakistan hapo February 18 2008 uliwashangaza wachunguzi wengi. Kinyume chake wasi wasi mkubwa uliokuwapo kwamba matokeo yangepangwa kama ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita, waungaji mkono wa rais Pervez Musharraf walibidi kukubali kipigo kikubwa. Chama cha Pakistan People's Party PPP, ambacho muda mfupi baada ya kuuwawa kwa Benazir Bhutto kilishinda uchaguzi, kiliunda serikali ya mseto chini ya waziri mkuu Yousuf Raza Gillani na kumlazimisha hatimaye Musharraf kuondoka madarakani. Majira ya joto mwaka huo huo mume wa marehemu Bhutto , Asif Zardari alichaguliwa kuwa rais. Lakini tathmini ya mwaka mmoja wa demokrasia inaonyesha wazi kuwa bado si nzuri. Hususan hali ya usalama katika maeneo ya mpaka na Afghanistan imezidi kuwa mbaya.


Kurejea kwa demokrasia nchini Pakistan baada ya karibu muongo mmoja wa utawala wa kijeshi ulikuwa , kulikaribishwa kwa matumaini makubwa mwaka mmoja kabla. Sio tu Wapakistan lakini hata jamii ya kimataifa ilikuwa imepoteza imani na Pervez Musharraf, mtu ambaye alikuwa amejilimbikizia madaraka, na kwa gharama yoyote ile abakie madarakani.

Wengi walikuwa na matumaini kuwa utawala wa kidemokrasi utafanikiwa hatimaye , kutokana na kuungwa mkono na wananchi na kuwahamasisha kupambana na watu wenye imani kali.

Lakini mwaka mmoja baadaye bado kuna hali ya shaka , ni kiasi gani jeshi limejiweka mbali na siasa.Kila wakati serikali ya kiraia inapaswa kuangalia nyuma, iwapo jeshi na idara ya ujasusi iliyojaa wanajeshi ya Inter-Services Intelligence , ISI kama inataka kuchukua hatua, hususan katika maeneo muhimu ya kisiasa kama uhusiano na nchi jirani ya India ama mapambano na wapiganaji nchini humo.

Mtaalamu wa masuala ya sayansi ya kisiasa mjini Berlin Wolfgang Merkel kutokana na hali hiyo , anaiweka Pakistan kuwa ni taifa la kidemokrasi ikiwa na mapungufu kadha.


Jeshi likiwa kama mhimili wa demokrasia, na iwapo uchaguzi huru utafanyika, lakini wawakilishi waliochaguliwa kwa kiasi fulani , huchukua madaraka mikononi mwao.Wengi wa wanasiasa nchini Pakistan manadai kuwa jeshi limerejesha nyuma demokrasia , na si mara ya kwanza katika historia ya Pakistan. Ahsan Iqbal ni katibu mkuu wa chama cha pili kikuu cha Muslim -League kinachoongozwa na Nawaz Sharif.


Kila dikteta alilazimishwa na wananchi kuachia madaraka kabla ya sauti za wanademokrasia kupaazwa. Kulikuwa na uchaguzi ambao kila dikteta alipaswa kuusimamia, haikuwa mapenzi yake, na hatimaye kila dikteta alipigwa vita na vyama vya kijamii, na ama alilazimishwa kujiuzulu ama alijitoa mwenyewe madarakani.


Kwa muda wa mwaka mmoja harakati za wananchi nchini Pakistan , zikiongozwa na majaji na mawakili , waliandamana dhidi ya Musharraf , kwa kuwa alimuondoa jaji mkuu wa mahaka katika madaraka. Mwaka mmoja baada ya uchaguzi serikali ya mseto baina ya chama cha People's Party na chama cha Muslim League cha Nawaz Sharif ulikuwa madarakani. Pia muungano huu usio wa kawaida wa vyama ambavyo kwa kawaida vinauhasama hali hiyo inachochea matumaini ya mwanzo mpya wa demokrasia. Chama cha Muslim League kimepoteza madaraka ya kuiongoza serikali, kwa kuwa kiongozi wa chama cha PPP, Zardari kiliendelea kuzuwia kurejeshwa madarakani kwa jaji mkuu wa mahakama.

Sekione Kitojo/ZR

►◄
  • Tarehe 18.02.2009
  • Mwandishi Sekione Kitojo
  • Chapisha Chapisha ukurasa huu
  • Kiungo https://p.dw.com/p/Gws7