Musharraf aondoa amri ya hali ya hatari | Habari za Ulimwengu | DW | 15.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Musharraf aondoa amri ya hali ya hatari

ISLAMABAD.Rais Pervez Musharraf wa Pakistan ameondoa amri ya hali ya hatari aliyoitangaza mapema mwezi uliyopita. Musharraf anategemewa kulihutbia taifa.

Waziri wa habari wa Pakistan Nisar Memon amesema kuwa Rais Musharraf amekwishatia saini sheria ya kuondoa amri hiyo.

Rais huyo wa Pakistan akitetea hali hiyo alisema kuwa ilikuwa ni muhimu katika kupambana na ongezeko wa ghasia na kushughulikia masuala ya sheria ambayo yalikuwa yakikwamisha shughuli za serikali.

Uchaguzi nchini Pakistan umepangwa kufanyika tarehe 8 mwezi ujayo ambapo mawaziri wakuu wawili wa zamani Bi Benazir Bhutto na Nawaz Sharif wanategemewa kushiriki.

Waziri wa habari wa nchi hiyo Nisar Memon amesema kuwa kwa kuondolewa amri hiyo ya hatari uchaguzi huo utaimarisha harakati za nchi hiyo kurejea katika demokrasi.

Wakati huo huo mshambuliaji wa kujitoa mhanga amejilipua katika kambi ya jeshi huko kaskazini magharibi mwa Pakistan na kuwaua watu watano.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com