Musharaf asema Marekani isithubutu kuvamia Pakistan
11 Januari 2008SINGAPORE
Rais wa Pakistan Pervez Musharraf amefahamisha kwamba hatua yoyote ya wanajeshi wa Marekani dhidi ya wanamgambo katika eneo la mpaka na Afghanstan itakayochukuliwa bila idhini yake itachukuliwa kama uvamizi.
Rais Musharraf ametoa matamshi hayo katika gazeti la Singapore la The Straits Times.Amesema serikali yake itapinga hatua yoyote ya wanajeshi wanaongozwa na Marekani katika maeneo hayo tete ya kuwasaka wanamgambo wakiislamu.Aidha rais Musharraf ameliambia gazeti hilo kwamba atajiuzulu ikiwa serikali mpya itakayokuja baada ya uchaguzi uliopangiwa kufanyika mwezi ujao itaamua kumtilia shaka.Pakistan imekuwa ikishinikizwa na Marekani kuwamaliza Alqaeda na wanamgambo wa Taliban wanaoaminika kuwa wanajificha katika maeneo hayo ya milimani karibu na mpaka wa Pakistan na Afghanstan.Hivi karibuni gazeti la New York Times nchini Marekani lilichapisha taarifa kwamba Marekani inafikiria kuanzisha opresheni kali za kijeshi katika eneo la Pakistan.