Mradi wa kinu cha nyuklia wakosolewa | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 28.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mradi wa kinu cha nyuklia wakosolewa

Wanasiasa nchini Ujerumani wamekosoa mpango wa Ufaransa wa kutaka kujenga kinu cha nyuklia nchini Libya.Mwenyekiti-mwenza wa chama cha upinzani cha Kijani nchini Ujerumani,Reinhard Bütikofer ameueleza mpango huo kama ni „harakati hatari za kizalendo."

Wanasiasa wengine kutoka vyama CDU na SPD vya serikali ya mseto ya Ujerumani wamesema,hatua ya Ufaransa inachukuliwa mapema mno na huenda ukawa hatari.

Wakati huo huo, Gernot Erler wa SPD,alie waziri wa dola katika wizara ya nje ya Ujerumani amesema:

“La kuulizwa hapo,ikiwa ni busara kufanya kazi zaidi na Gaddafi,kazi hiyo inapohusika na teknolojia ya nyuklia na silaha au upo uwezekano mwingine pia.“

Siku ya Alkhamisi,Rais wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy alitia saini taarifa ya maelewano pamoja na Libya,ikihusika na makubaliano ya kujenga kinu cha nishati ya nyuklia.

Hatua hiyo imechukuliwa miaka minne kufuatia tangazo la Rais wa Libya, Muammar Gaddafi,kufutilia mbali miradi ya nchi hiyo,kutengeneza silaha za nyuklia,kemikali na kibiolojia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com