Mkuu wa chama cha soka Rwanda akamatwa | Matukio ya Kisiasa | DW | 11.06.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkuu wa chama cha soka Rwanda akamatwa

Alikuwa amekwenda Afrika Kusini kushuhudia michuano ya komba la dunia la kandanda

default

Rais Paul Kagame wa Rwanda

Jeshi la Rwanda limetangaza kuwa limemkamata na kumtia jela Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini humo, FERWAFA, Brigadia Jenerali John Bosco Kazura. Msemaji wa jeshi hilo ametangaza mjini Kigali kuwa rais huyo wa FERWAFA alifanya makosa ya kwenda nje ya nchi bila kibali cha wakubwa wake. Jenerali Kazura inasemekana alikuwa amekwenda Afrika ya Kusini kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa kombe la dunia ambalo limeanza leo. Yeye ni afisa wa tatu wa cheo cha jenerali kutiwa kizimbani kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita.

Daniel Gakuba anayo maelezo zaidi kutoka Kigali.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

 • Tarehe 11.06.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/NolS
 • Tarehe 11.06.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/NolS
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com