Mkutano wa chama cha Leba | Magazetini | DW | 24.09.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Mkutano wa chama cha Leba

Waziri mkuu wa Uingereza Brown aokoka Manchester.

Bw,Brown na Obama

Bw,Brown na Obama

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo wamechambua mada nyingi tangu za ndani ya nchi hata nje yake:Wamechambua juu ya msukosuko wa mabaneki nchini Marekani na iwapo seneta Obama au MCcain wana ujuzi na uwezo wa kukifumbua kitandawili chake.Wamechambua mkutano mkuu wa chama cha Leba nchini Uingereza huko Manchester na hatima ya waziri mkuu Gordon Brown lakini pia kisa cha mwanafunzi aliefyatua jana risasi kuuwa wanafunzi 10 nchini Finnland.

Gazeti la Neue Presse juu ya mauaji ya jana ya holela holela laandika :

Katika mkasa huu mawazo ya kuwashughulikia wanyonge na wenye shida ambayo Finnland inasifiwa yameshindwa kufanya kazi .Na hasa baada ya kugunduliwa video ilionesha kitisho cha nia ya kuua.......Mtandao wa Internet unatumiwa hii leo na wauaji holela holela kama hawa kama aina ya kujikomboa binafsi kutoka shida na kero walizonazo maishani.Wanapanga mauaji yao wakifuata mfumo maalumu-mfumo wa yule mfyatuaji risasi alieuwa wanafunzi kadhaa katika chuo kikuu cha Columbine,Marekani 1999.

Kinachosaidia ,lasema gazeti katika hali hii,ni kuwa macho na hata ukibidi kutoa onyo kwa hatari isiokuwapo.Humu nchini hali hii imetambuliwa zamani-laandika Neue Presse kutoka Hannover.

Likiendeleza mada hii, gazeti la Thuringische Landeszeitung kutoka Weimer laandika:

"Kuvizia na kupiga chenga ni sehemu ya mikakati ya kila mwanamgambo aliejizatiti kwa kila hali na asiejali maisha tangu yake hata ya weengine.Haki ya kumiliki silaha inawasadia watu kama hawa.Hali hii itasalia hivyo hata ikiwa baada ya mkasa huu vilio vitasikika kutia makali sheria za kumiliki silaha......Bila kuchukua hatua kali hakuna kitakachobadilika."

Hilo ni Thuringische Landeszeitung kutoka Weimer.

Likitugeuzia mada gazeti la Dresdner Neuste Nachrichten lazungumzia hatima ya waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown katika mkutano wa chama cha Leba huko Manchester .Linaandika kwamba Bw. Gordon Brown angeweza hata kutoa hotuba mbaya zaidi kuliko aliyotoa na akaokoka .Gazeti laongeza:

"Kwa kila njia mwanzoni mwa mkutano ilibainika wazi:Chama ambacho kilitaka kumpiga kumbo Bw. Brown,kilikwisha uma meno kubakia nae.Kwani, chama hakina kiongozi bora wakati huu.Tony Blair mpya haonekani.Yaonesha ili kuzuwia kutumbikia shimoni kwa chama cha Leba ndiko kuliko kiunganisha kitu kimoja. Na ili kuepusha kupoteza madaraka ,chama cha Leba kinapepea nje bendera ya Umoja na mshikamano...."

Gazeti la Badische Nueste Nachrichten laandika kwamba, Bw.Brown anajua vipi kupania na kuviringa ngumi kupigana. Kwani, kama alivyotarajiwa, hakufaulu kiongozi huyu wa chama cha Leba kuwabakishia wenzake chamani matumaini ya mwisho.Lakini, Bw.Brown juu ya hivyo,aligundua maneno matamu ya "kumtoa nyoka pangoni "na kujiokoa.

Gazeti la Schwabische zeitung limemgeukia yule mwenye uchu wa kutaka na mapema kurithi wadhifa wa Bw.Brown:

"Huko Manchester watetezi wa kiti cha Bw.Brown na hasa waziri wa nje David Miliband ,hawakufanikiwa kutimiza shabaha yao.Kwani, ilibainika ni mapema kujaribu kumtia munda Bw.Brown licha ya kwamba wabunge 349 wa chama cha Leba wana hofu kubwa kupoteza viti vyao katika uchaguzi ujao.

Mwishoe, gazeti la Financial Times Deutschland likizungumzia msukosuko wa banki nchini Marekani laandika:

"Hakuna hata mtetezi mmoja wa wadhifa wa urais wa Marekani mwenye maarifa ya kutosha ya maswali ya fedha.Na hakuna aliejitokeza na ufumbuzi mzuri hadi sasa.Si Bw.Obama wala McCain.Wananchi wa Marekani watasubiri sana dawa mjarabu ya mzozo huu,kwavile, hakuna kati yao atakaeweza kutimiza ahadi atazotoa kwao atakapoingia Ikulu mjini Washington."