Mjerumani mwenye asli ya kipakistan akamatwa kwa Ugaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 16.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mjerumani mwenye asli ya kipakistan akamatwa kwa Ugaidi

Mtu huyo anatuhimiwa kushirikiana na magaidi wa Alqaeda

BERLIN

Raia wa Ujerumani mwenye asili ya kipakistan amekamatwa kwenye mji wa kusini mashariki mwa Ujerumani baada ya kushukiwa kufanya kazi na mtandao wa kigaidi wa Alqaeda.Afisi ya Mshatki mkuu wa serikali imtoa taarifa ikisema kwamba mtu huyo mwenye umri wa miaka 45 alifanya ziara mara nne ya kwenda eneo la mpaka kati ya Pakistan na Afghanstan ambako alipeleka kiasi cha Euro elfu 4 kwa kundi la ASlqaeda kwa ajili ya shughuli zao.Aidha inadaiwa mshukiwa huyo wa ugaidi alitumia zira hizo ziliyofanyika kati ya mwezi Aprili mwaka 2005 na mwezi Juni mwaka 2007 kuingiza kimagendo vifaa vya redio na vifaa vya darubini kwa kundi la ugaidi.Halikadhalika mshukiwa huyo anashutumiwa kwa kuhudhuria mafunzo ya kutumia mabomu kwenye kambi moja nchini Pakistan.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com