1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri inapinga vikwazo ziada dhidi ya Sudan

18 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHs

Cairo:

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Misri Ahmed Aboul Geith anapinga vikwazo ziada dhidi ya Sudan.Akizungumza na waandishi habari mjini Cairo,waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Misri ametahadharisha dhidi ya “hatari ya kushadidia vikwazo dhidi ya Sudan".Balozi wa Uengereza katika umoja wa Mataifa Emyr J. Parry alitishia mapema wiki iliyopita,Sudan itawekewa vikwazo vyengine na baraza la usaalama ikiwa nchi hiyo haitajifungamanisha na ahadi ilizotoa kuruhusu vikosi vya pamoja vya Umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika viwekwe Darfour.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa misri Ahmed Aboul Gheith amesema ametuma risala za dharura kwa wanachama wa kudumu wa baraza la usalama,ofisi ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa,Umoja wa Afrika na Umoja wa ulaya,kuwasihi watilie maanani barua aliyoandikiwa hivi karibuni katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon na rais Omar el Bashir wa Sudan.