Mipango ya kuchoma Koran tukufu yaahirishwa | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 10.09.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Mipango ya kuchoma Koran tukufu yaahirishwa

Uamuzi huo umetangazwa na Mchunganji Terry Jones wa Kanisa moja nchini Marekani, aliyepanga kuchoma moto nakala za Koran tukufu hapo kesho.

Mchungaji Terry Jones akiwa na Imamu Muhammad Musri wa Kituo cha Jumuiya ya Kiislamu Florida.

Mchungaji Terry Jones akiwa na Imamu Muhammad Musri wa Kituo cha Jumuiya ya Kiislamu Florida.

Mchungaji wa Kanisa moja nchini Marekani aliyepanga kuchoma moto Koran tukufu hapo kesho, ameahirisha mipango hiyo. Kitendo hicho cha Mchungaji Terry Jones cha kutaka kuchoma nakala za kitabu cha Koran tukufu kililaaniwa na jumuiya kimataifa.

Akizungumza na waandishi habari, Mchungaji Jones alisema uamuzi huo unatokana na mpango wa viongozi wa kituo cha Kiislamu kinachotarajiwa kujengwa katika eneo yalikotokea mashambulio ya kigaidi mjini New York, Septemba 11 mwaka 2001, kuhamisha eneo la ujenzi wa kituo hicho.

Hata hivyo taarifa hizo zimekanushwa na duru za karibu za kituo hicho cha kidini. Tangazo la kuchoma moto nakala za kitabu kitakatifu cha Koran kimesababisha kufanyika maandamano katika nchi mbalimbali za Kiislamu.

Ikulu ya Marekani ilimtolea wito Mchungaji Jones kutochoma Koran tukufu kwa hofu kuwa kitendo hicho kinaweza kusababisha mashambulio ya kujitoa mhanga dhidi ya Wamarekani ikiwa ni katika kulipiza kisasi.

 • Tarehe 10.09.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/P8kn
 • Tarehe 10.09.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/P8kn
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com