1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Medvedev asema Moscow italipa kisasi vikwazo vya magharibi

Lilian Mtono
24 Februari 2024

Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev amesema Moscow itaangazia namna ya "kulipiza kisasi" kufuatia kiwango kikubwa cha vikwazo vya kiuchumi vilivyotangazwa na mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani.

https://p.dw.com/p/4cpVL
Dmitry Medvedev
Dmitry MedvedevPicha: Yekaterina Shtukina/Sputnik Government/AP/dpa/picture alliance

Medvedev ameandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba ni wazi sababu iliyo nyuma ya vikwazo hivyo ni kuwaumiza raia wa Urusi na kwa maana hiyo watahakikisha wanalipa kisasi kwa namna inavyowezekana.

Amesema mataifa yote ya magharibi ni maadui zao.

Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza vikwazo vipya 500 dhidi ya Urusi jana Ijumaa ikiwa ni mwaka wa pili tangu Urusi ilipoivamia Ukraine. Biden ameapa kuendeleza shinikizo kuzuia vita vya rais wa Urusi Vladimir Putin.