Mecca. Mahujaji wakamilisha swala ya hija katika mlima Arafat. | Habari za Ulimwengu | DW | 30.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mecca. Mahujaji wakamilisha swala ya hija katika mlima Arafat.

Nchini Saudi Arabia , zaidi ya mahujaji milioni mbili katika mlima Arafat nje kidogo ya mji mtakatifu wa Mecca wameshiriki katika swala siku nzima ikiwa ni sehemu ya Hija ya mwaka huu.

Kwa mujibu wa utaratibu Mtume Muhammad alitoa hotuba yake ya mwisho katika mji huo ulioko jangwani kiasi cha miaka 1,400 iliyopita.

Utaratibu huo ambapo mahujaji wanaomba msamaha kwa dhambi zao ni tukio la mwisho la kiroho kwa ajili ya Hija ambayo ilianza siku ya Alhamis na kumalizika siku ya Jumatatu. Hatua kadha mpya za usalama zimechukuliwa mwaka huu, zenye lengo la kuepusha mkanyagano ambapo katika siku za nyuma ulisababisha mamia ya watu kuuwawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com