Matatizo ya kuandikishwa kwa wapiga kura Zanzibar | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.04.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Matatizo ya kuandikishwa kwa wapiga kura Zanzibar

Tume ya Uchaguzi Visiwani Zanzibar ZEC imesema haitorefusha zoezi la uandikishaji wa wapiga kura, licha ya malalamiko kuwa zaidi ya watu laki moja na nusu hawajajiandikisha.

Kulingana na Mwenyekiti wa ZEC Khatibu Mwinyichande, tume hiyo haiwezi kuongeza muda kwa sababu bajeti iliyotengewa zoezi hilo imemalizika. Lakini wapinzani wanaliangalia kwa sura tofauti suala hili. Hujuma za kisiasa. Je nini msimamo wa chama cha CUF kuhusiana na suala hili. Munira Muhammad alizungumza na Ismail Jussa, Mbunge maalum na pia Afisa wa ngazi ya juu wa CUF. Na kwanza anaelezea msimamo wa chama hicho kuhusiana na tangazo hilo la tume ya uchaguzi ya Zanzibar.

Mwandishi: Munira Muhammad

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com