Mataifa ya Ulaya kuanzisha tena matumizi ya AstraZeneca | Siasa na jamii | DW | 19.03.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Siasa na jamii

Mataifa ya Ulaya kuanzisha tena matumizi ya AstraZeneca

Mataifa makubwa barani Ulaya yamesema yataanzisha upya matumizi ya chanjo ya AstraZeneca baada ya chombo cha udhibiti wa kitabibu cha Ulaya kusema chanjo hiyo ni salama na inafanya kazi vizuri.

Mataifa makubwa barani Ulaya yamesema yataanzisha upya matumizi ya chanjo ya AstraZeneca baada ya chombo cha udhibiti wa kitabibu cha Ulaya kusema chanjo hiyo ni salama na inafanya kazi vizuri.

Na wala haina uhusiano na athari za kuganda kwa  damu baada ya matumizi yake. Kauli hiyo inafuatia ile ya shirika la afya duniani WHO na lile la uangalizi wa afya la Uingereza kwa pamoja kusema chanjo hiyo ni salama.

Muda mfupi baada ya Shirika la Uangalizi wa Madawa la Ulaya (EMA) kutangaza usalama wa AstraZeneca mataifa ya Ulaya yaliotangaza kuendelea na chanjo hiyo ni pamoja na Ujerumani, Ufaransa, Uhispania, Italia, Uholanzi, Ureno, Lithuania, Latvia, Slovenia na Bulgaria.