Mashauri ya utafuta amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yaanza Mjini Nairobi. | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.12.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mashauri ya utafuta amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yaanza Mjini Nairobi.

Mazungumzo ya kutafuta amani yanayozileta pamoja pande mbili kwenye mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanafanyika katika makao makuu ya Umoja wa mataifa mjini Nairobi Kenya.

default

Kiongozi wa kundi la waasi Jemedari Laurent Nkunda asisitiza kufanya mashauriano na Rais Joseph Kabila


Mkutano huo unaotarajiwa kumalizika siku ya Jumatano wiki hii, ni kwanza kunawaleta pamoja waakilishi wa serikali ya Rais Joseph Kabila na kundi la muasi Laurent Nkunda.


Mashauriano hayo yalikumbwa na tisho la kuvurugwa baada ya wafusia wa Nkunda kutisha kujiondoa .


Tisho hilo linafuatia hatua ya serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo mwishoni mwa wiki, ya kuyaalika makundi mengine 20 ya waasi nchini humo, kuhudhuria mashauriano hayo yanayofadhiliwa Umoja wa Mataifa, kutafuta suluhisho la kudumu kwa mapigano yanayoendelea katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.


Huu ni mkutano wa kwanza unaozileta pamoja pande mbili zinazozozana nchini Congo, baada ya upande wa Jenerali Nkunda kususia duru ya kwanza ya mashauri hayo yaliyofanyika mjini Nairobi mwezi uliopita.


Msapigano nchini Congo tayari yamesababisha vifo vya maelfu ya raia wasio na hatia na wengine wasiopungua 250,000n kuachwa bila makao.


Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa kwenye mzozo huo Olusegun Obasanjo, aliusihi upande wa Laurent Nkunda kushiriki mashauriano hayo, akisema kuwa mkutano huo unafungua pazia la kupatikana kwa amani nchini Congo.Waandishi wa habari hawakuruhusiwa kwenye mashauriano hayo yanayofanyika

Ujumbe wa kundi la muasi Jenerali Laurent Nkunda la CNDP,ulisema kabla ya kuanza kwa mashauriano hayo kwamba hauko tayari kufanya mazungumzo hayo na makundi mengine ya waasi yaliyoalikwa.


Msemaji wa kundi hilo la CNDP, Rene Abandi alisema kuwa mashauriano hayo yalikuwa baina ya serikali na kundi lake na kwamba hawawezi kukaa meza moja na waasi wa kundi la Mai Mai, wanaoamini kuwa ni wafuasi wa serikali ya Rais Joseph Kabila.


Mnamo siku ya Jumapili waziri wa habari nchini Congo Lambert Mende alitanga kujumuishwa kwa makundi mengine ya waasi kwenye mazungumzo hayo.


Wafuasi wa Laurent Nkunda hawakufurahishwa na tangazo hilo na wanashaka iwapo mkutano wa Nairobi utakuwa na mafanikio yoyote.

Waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Kenya Moses Wetangula alisema kuwa Kenya, imewahi kuongoza na kufanikisha mashauriano ya amani hapo mbeleni na anaimani kuwa mkutano huo utaleta amani nchini Congo.


Mashauriano hayo yamepongezwa na jamii ya kimataifa yakitajwa kuwa mwelekeo ufaao katika kumaliza vita nchini Congo.


Waasi wa Laurent Nkunda walitangaza kusitisha mapigano baada ya kuuzingiza mji wa Goma ambao ni mji mkuu wa Jimbo la Kivu kaskazini mnamo mwezi Oktoba.

Hali hiyo imedumishwa na kupelekea kuwepo kwa hali ya utulivu katika eneo hilo la Kivu Kaskazini, ingawa kumetoka mapigano ya mara kwa mara baina ya kundi la waasi wa Mai Mai na kundi jingine la waasi wa Kihutu na lile linaloongozwa na Laurent Nkunda katika jimbo hilo lenye utajiri mkubwa wa dhahabu, na Almasi.


Wakati hayo yakiendelea mjini Nairobi,mkutano wa viongozi wa jumuiya ya Ulaya unaoendelea mjini Brussel Ubeligiji, wanajadili uwezekano wa kutumwa kikosi cha wanajeshi zaidi wa kuhifadhi amani nchini Congo kusaidia juhudi la kikosi cha umoja wa mataifa kilichoko katika eneo hilo.


Hata hivyo,bado kunamgawanyiko miongoni mwa wajumbe hao, iwapo kikosi hicho kinapasa kutumwa nchini kabla ya kuwasili kwa kile cha wanajeshi 3,000 wa umoja wa mataifa nchini humo.

 • Tarehe 08.12.2008
 • Mwandishi Eric Kalume Ponda
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GBoL
 • Tarehe 08.12.2008
 • Mwandishi Eric Kalume Ponda
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GBoL
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com