1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yawaua 21 Gaza City

23 Novemba 2025

Mamlaka ya ulinzi wa raia katika Ukanda wa Gaza, imesema watu 21 wameuwawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulizi kadhaa ya angani kutoka Israel,

https://p.dw.com/p/544RN
Gaza City 2025 | Mgogoro wa Mashariki ya Kati
Mashambulizi ya Israel dhidi ya wapalestina yaliyowaua watu 21 Gaza City, yalikuwa mabaya kuwahi kushuhudiwa tangu makubaliano hayo yalipoanza kutekelezwa Picha: Majdi Fathi/NurPhoto/picture alliance

Hayo yanajiri wakati Hamas na Israel wakilaumiana kuhusu ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Mashambulizi hayo yaliyotokea jana Jumamosi (22.11.2020), yalikuwa mabaya kuwahi kushuhudiwa tangu makubaliano hayo yanayosimamiwa na Marekani, yalipoanza kutekelezwa Oktoba 10, baada ya miaka miwili ya vita. 

Jeshi la Israel limesema lilikuwa linajibu mashambulizi kutoka kwa Hamas dhidi ya wanajeshi wake huku Hamas nayo ikikanusha madai hayo na kusema Israel inatafuta sababu ya kushambulia.

Kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas, wapalestina 312 wameuawa na Israel tangu makubaliano hayo dhaifu yalipoanza kutekelezwa.