1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulio ya Mumbai na matokeo yake

Oumilkher Hamidou30 Novemba 2008

Waziri nwa mambo ya ndani na mkuu wa idara ya usalama wa taifa wajiuzulu

https://p.dw.com/p/G6JR

New-Delhi:

Mshauri wa usalama wa taifa nchini India  M.K.Narayanan amejiuzulu kufuatia mashambulio ya kigaidi katika mji mkuu wa kiuchumi Mumbai.Huyo ni kiongozi wa pili kujiuzulu baada ya waziri wa mambo ya ndani kuwasilisha maombi yake ya kujiuzulu mapema hii leo.Shivraj Patil amesema katika hati aliyomkabidhi waziri mkuu Manmohan Singh,"ana jukumu la kimaadili "kwa mashambulio yaliyotokea.Waziri mkuu Singh amekubali uamuzi huo na kumchagua waziri wa fedha kushikilia wadhifa huo wa waziri wa mambo ya ndani.Wizara hiyo ya fedha  itakua kwa sasa ikisimamiwa na waziri mkuu Manmohan Singh.Serikali inalaumiwa kwa uzembe wa idara zake za upelelezi.Wahindi wanalalamika mashambulio hayo ya kigaidi yameendelea kwa siku tatu kabla ya kushindfwa nguvu na vikosi maalum.Gaidi pekee ambae hajauwawa amekiri walikuaa na mafungamano na kundi la waasi wa itikadi kali la Lashkar e-Taiba nchini Pakistan.Mashambulio ya kigaidi ya Mumbai yamegharimu maisha ya watu karibu 200 na wengine 300 kujeruhiwa.