1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yapitisha mswada kwa ajili ya Ukraine na Israel

14 Februari 2024

Baraza la Seneti la Marekani limeupitisha mswada juu ya msaada zaidi wa fedha kwa ajili ya Ukraine. Msaada huo unaijumuisha pia Israel na Taiwan. Kulingana na mswada huo, Ukraine inatarajiwa kupatiwa dola bilioni 60.

https://p.dw.com/p/4cO5d
Washington, Marekani | Rais Joe Biden wakipena mikono na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais Joe Biden akimsabahi Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Drew Angerer/Getty Images

Kulingana na mswada huo, Ukraine inatarajiwa kupatiwa dola bilioni 60. Israel itapatiwa dola bilioni 14 na fungu jingine litakwenda Taiwan.

Hata hivyo wajumbe wa chama cha Republicans wamesema watauangusha mswada huo utakapowasilishwa mbele ya baraza la wawakilishi.

Soma pia:Marekani: hakuna mwaliko wa NATO kwa Ukraine katika mkutano wa kilele wa Julai

Wabunge wa chama cha Republican ndiyo wengi. Kwa muda wa miezi kadhaa sasa wajumbe wa chama hicho cha Republican wamekuwa wanazuia kupelekwa msaada zaidi kwa Ukraine.