Marekani yaiwekea Sudan vikwazo. | Matukio ya Kisiasa | DW | 29.05.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Marekani yaiwekea Sudan vikwazo.

Rais George Bush wa Merekani leo mchana alitangaza vikwazo zaidi, dhidi ya Serekali ya Sudan, ya Rais Omar Hassan El-Bashir

Rais George Bush wa Marekani

Rais George Bush wa Marekani

Rais Bush amesema hii imefatia ukaidi wa viongozi wa Sudan, kuendelea kuunga mkono, Vikosi vya usalama nchini humo, kuzidi kuwanyanyasa wakazi wa eneo la Darfur Magharibi mwa Sudan.

Katika hutuba yake fupi alieitoa ,Rais George Bush wa Merekani amesema, vikwazo hivyo vinapiga marufuku, Mashirika ya Kimerekani na watu binafsi, ria wa US; kufanya biashara na Sudan.

Ameongeza kusema hali ya usalama katika eneo la Darfur haijabadilika kitu, unyanyasaji na mauaji ya halaiki bado unaendelea dhidi ya watu wa Darfur.

Rais Bush ameitaka Serekali ya Rais Omar Hassan El-Bashir ikubali vikosi vya kulinda Amani vya UN vichukue jukumu la kuwalinda watu wa Darfur.

Kwa upande mwengine vikwazo hivi vya Merekani dhidi ya Serekali ya Khartoum, inamaanisha kua, mashirika ya kibiashara ya Sudan hayatoweza kutumia sarafu ya Merekani (Dollar) katika biashara yao kimataifa.

Hii na mara ya pili Serekali ya US ikiiwekea vikwazo Serekali ya Sudan, mara ya mwanzo ulikua mwaka 1997 .

Serekali ya Uchina ambae ni mshirika mkuu wa kibiashara na Sudan imesema, vikwazo hivyo vya US dhidi ya Sudan havitosaidia kitu isipokua kuukuza mzozo wa Darfur kuliko kuutatua.

Mjumbe maalum wa Serekali ya Uchina katika mzozo wa Darfur, Bw Liu Guijin, ambae amekueko Darfur hivi karibuni,amesema na namnukuu;

Matatizo ya Sudan yanasababishwa na umaskini na kutokueko maendeleo, na ikiwa mambo hayo mawili yatapatiwa ufumbuzi ,

Nna hakika, amani na maendeleo itapatikana Darfur, na ndio mana tuna ushirikiano wa kibiashara na Sudan, njia peke inayoweza kuisaidia Sudan, kumaliza mzozo wa Darfur.

Ijuma iliopita Baraza la usalama la UN lilipendekeza jeshi la vikosi vya UN lifanye kazi kwa pamoja na vikosi vya jeshi la Umoja wa Afrika kuwalinda wakaazi wa Darfur na pia kutumia nguvu kuzuwia machafuko yanapotokea.

Inavoonyesha Uchina huenda ikatumia kura yake ya veto, ikiwa US itafaulu kulishawishi baraza la UN kuiwekea vikwazo Sudan.

Watu zaidi ya 200 Elfu wamepoteza maisha yao katika mzozo wa Darfur tangu ulipoanza mwaka 2003, wapiganaji wanaoitwa Janjawid ambao inasemekana wanasaidiwa na Serekali ya Sudan, wakipigana dhidi ya kundi la Sudan Liberation Movement,linalotaka haki zaidi kwa watu wa Darfur.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nchi za njee wa Ufaransa, Bernard Kouchner amesema wanasubiri uamuzi wa Rais Nicolas Sakorzy ili Ufaransa ianze kutoa misaada ya kibinaadamu kwa watu wa Darfur.

 • Tarehe 29.05.2007
 • Mwandishi Mutasa Omar
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHDZ
 • Tarehe 29.05.2007
 • Mwandishi Mutasa Omar
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHDZ

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com