1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaionya China dhidi ya ushindi wa Urusi, Ukraine

Mohammed Khelef
10 Aprili 2024

Marekani imeonya China kwamba itaibebesha dhamana ikiwa Urusi itapata mafanikio kwenye vita vyake nchini Ukraine, baada ya Beijing kurejelea ahadi yake ya kuimarisha uhusiano na Moscow

https://p.dw.com/p/4ebDi
USA Washington - Kurt Campbell
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayehusika na Asia, Kurt Campbell,Picha: picture-alliance/Kyodo

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayehusika na Asia, Kurt Campbell, amesema kwa nchi yake, suala la kudumisha amani na utulivu barani Ulaya ni mojawapo ya majukumu muhimu ya kihistoria.

Lavrov ziarani China

Wakati huu Moscow inaporejesha mashambulizi yake dhidi ya Ukraine huku kukiwa na mkwamo wa kuidhinishwa kwa msaada wa kijeshi kwenye Bunge la Marekani, Campbell ameonya kwamba mafanikio ya Urusi nchini Ukraine yanaweza kuchafuwa mizani ya madaraka kwa kiwango ambacho hakikubaliki.

Marekani imekuwa ikitishia kuiwekea vikwazo Beijing ikiwa itachukuwa hatua za kuisaidia Urusi.