Marekani kutuma wanajeshi zaidi Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 10.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Marekani kutuma wanajeshi zaidi Afghanistan

WASH INGTON

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates anafikiria kutuma wanamaji wa ziada 3,000 nchini Afghanistan.

Msemaji wa wizara ya ulinzi amesema kuongeza wanajeshi hao wa Marekani kunakusudia kuimarisha vikosi vilioko nchini Afghanistan kabla ya mashambulizi yanayotazamiwa ya kundi la Taliban ya kipindi cha majira chipukizi.Wanamaji hao wanatarajiwa kuziba pengo la uhaba wa takriban wanajeshi 7,500 walioko katika mapambano nchini Afghanistan. Hivi sasa kuna wanajeshi 26,000 nchini Afghanistan wengi wao wakiwa chini ya Kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama ISAF kinachoongozwa na Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi NATO.Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com