1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Marekani, Kenya zatazamia kuimarisha uhusiano wa kibiashara

25 Mei 2024

Marekani na Kenya zimesema jana kuwa zitafanya duru mpya ya mazungumzo ya biashara mwezi ujao, baada ya duru ya hivi karibuni iliyofanyika mjini Washington.

https://p.dw.com/p/4gGru
Marekani| Joe Biden amkaribisha William Ruto
Rais Joe Biden akimkaribisha William Ruto katika Ikulu ya White House, Mei 22, 2024.Picha: Yuri Gripas/CNP/picture alliance

Marekani na Kenya zimesema jana kuwa zitafanya duru mpya ya mazungumzo ya biashara mwezi ujao, wakati mataifa hayo mawili yakipigia debe makubaliano mapya ya biashara na yakitazamia kuimarisha uhusiano wa kiuchumi.

Rais wa Kenya William Ruto alikuwa mjini Washington kwa ziara ya kitaifa wakati Ikulu ya White House ilipoahidi ushirikiano mpya kuhusu teknolojia, usalama na msamaha wa madeni kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.

Soma pia: Biden, Ruto waahidi kulinda demokrasia Afrika na kwingineko

Rais Ruto aliahidi kurahisisha ufanyaji biashara nchini Kenya wakati akiwavutia wafanyabiashara kuwekeza nchini mwake.

Waziri wa biashara wa Marekani Gina Raimondo aliwahimiza viongozi wa biashara kuendeleza kasi baada ya matukio ya wiki hii, na kuwataka waingie makubaliano kuwekeza Kenya na Afrika kwa ujumla.

Ofisi ya Mwakilishi wa Biashara wa Marekani ilisema mataifa hayo mawili yatafanya duru ya sita ya majadiliano mjini Mombasa kuanzia Juni 3 hadi 7 baada ya mazungumzo ya mjini Washinton mwezi huu.