1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kuipandisha Kenya hadhi ya mshirika muhimu

24 Mei 2024

Rais wa Marekani Joe Biden amesema jana kuwa ataifanya Kenya kuwa mshirika mkuu asiye mwanachama wa jumuiya ya NATO.

https://p.dw.com/p/4gDYE
MArekani | Joe Biden ampokea William Ruto
Biden alimpokea Ruto katika ikulu ya White HousePicha: Susan Walsh/AP Photo/picture alliance

Rais Biden alitoa ahadi hiyo wakati alipomkaribisha rais William Ruto kwa ziara ya kitaifa iliyolenga kukabiliana ushawishi wa Urusi na China barani Afrika.

Biden alisema hatua hiyo inatimiza miaka ya ushirikiano dhidi ya makundi ya Dola ya Kiislamu na Al-Shabaab nchini Somalia.

Hatua hiyo itaifanya Kenya kuungana na mataifa mengine 16 yenye hadhi hiyo, yakiwemo Israel, Brazil na Ukraine, na hivyo kuimarisha ushirikiano wa kijeshi la kidiplomasia, ingawa hakutakuwa na makubaliano rasmi ya usalama.

Ziara ya Ruto Marekani ina maslahi gani?

Biden pia aliishukuru Kenya kwa kukubali kuongoza kikosi cha polisi wa kimataifa nchini Haiti, ambako miezi kadhaa ya magenge ya uhalifu imeliacha taifa hilo dogo la Karibia katika mzozo wa kisiasa na kiutu.