Magazetini.
16 Septemba 2009Wahariri wengi leo wanazungumzia mkasa
uliotekea kwenye kituo cha treni cha mjini
Munic ambapo muungwana mmoja alipigwa
na vijana wawili na kuuawa.Wahariri hao pia
wanatoa maoni yao juu ya mgogoro wa
nyuklia wa Iran.
Mhariri wa gazeti la Ostee Zeitung
anamkumbuka Patrick Swayze.
Jumamosi iliyopita vijana wawili walimpiga na kumwuua mfanyabiashara mmoja aliekuwa na umri wa miaka 50 kwenye kituo cha treni cha mjini Munic. Sababu ni kwamba mfanyabiashara huyo alijaribu kuwalinda watoto ili wasisumbuliwe na vijana hao wawili.
Juu ya mauaji hayo gazeti la Dithmarscher Landeszeitung linasema, sasa baada ya vijana hao wawili kumpiga na kumwuua mfanyabiashara huo, wanasiasa wanataka sheria ziwe kali zaidi.
Lakini mhariri wa gazeti hilo anasema adhabu kali hazitawasumbua wauaji hao.
Naye Mhariri wa gazeti la Emder Zeitung anakubaliana na hoja hiyo lakini anaeleza kuwa pana ushahidi unaoenyesha kwamba sheria kali peke yake hazitazuia matendo ya kutumia nguvu miongoni mwa vijana fulani.
Mhariri anasema polisi zaidi wanahitajika ili kuzuia vitendo vya ushari.
Katika maoni yake gazeti la Braunschweiger linasema vijana wauaji kama hao wawili lazima wakomeshwe. Lakini wajibu huo usiwe wa mwananchi mmoja peke yake.
Gazeti hilo pia linatilia maanani ulazima wa kuongeza idadi ya polisi ili kulinda usalama wa wananchi.
Gazeti la Münchner Merkur leo
linazungumzia mvutano baina ya Iran na nchi
za magharibi kuhusiana na mpango wa
nyuklia.Gazeti hilo linaeleza kwamba hadi
sasa hakuna dalili zozote juu ya kutatuliwa
kwa mgogoro huo.
Mhariri huyo anasema ikiwa Iran itaendelea na ukaidi nchi za magharibi zitapaswa kujiuliza iwapo zitakuwa tayari kuona taifa lenye silaha za nyuklia likizuka katika mashariki ya kati.?
Au nchi hizo zitachukua hatua kali?
Gazeti la Münchner Merkur linasema, ikiwa nchi za magharibi zitaamua kuchukua hatua hizo kali, Israel pia itapaswa ishiriki katika uamuzi ,kwa sababu Israel ndiyo itakayotishiwa.
Gazeti la Ostee Zeitung linatoa salam za
rambi rambi juu ya kifo cha mcheza senema
maaruf Patrick Swayze aliefariki jana
kutokana na maradhi ya saratani ya
kongosho.
Gazeti linasema mwigizaji huyo atakumbukwa kwa umahiri wake katika kucheza dansa.
Gazeti linakumbusha juu ya filamu inayoitwa dirty dancing ya Patrick Swayze ambayo kila mtu alitaka kuiona mwaka 1989.
Mwandishi /Mtullya-Deutsche Zeitung.
Mhariri/Othman,Miraj