Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani. | Magazetini | DW | 10.07.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

Katika maoni yao leo,wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanazungumzia juu ya kutekwa nyara watalii wa kijerumani nchini Uturuki.

Bendera ya chama cha PKK kinachopigania haki za wakurdi nchini Uturuki.

Bendera ya chama cha PKK kinachopigania haki za wakurdi nchini Uturuki.

Magazeti ya Ujerumani leo yanazungumzia juu ya kutekwa nyara watalii wa kijerumani nchini Uturuki.

Magazeti hayo pia yanatoa maoni kuhusu mkutano wa nchi nane tajiri uliofanyika nchini Japan.
Kuhusu kutekwa nyara watalii wa kijerumani nchini Uturuki, wahariri wanajaribu kuweka mwambatano baina ya tukio hilo na harakati za wakurdi wanaopigania haki ya kujiamulia mambo yao wenyewe nchini Uturuki.

Kwa mfano gazeti la Flensburger linasema, chama kinachopigania haki za wakurdi nchini Uturuki kina fedha za kutosha. Ndiyo kusema ikiwa wao ndiyo waliowateka nyara wajerumani hao,basi wamefanya hivyo kwa sababu za kisiasa na siyo kwa ajili ya fedha.


Gazeti la Dresdener Neueste Nachrichten pia linazungumzia kadhia hiyo kwa kutilia maanani kwamba , kwa muda mrefu serikali ya Uturuki imekuwa inakanusha kuwapo tatizo la wakurdi nchini.

Lakini mhariri wa gazeti hilo anaeleza kuwa siasa hiyo ilifikia mwisho baada ya wakurdi kupata sehemu yao ambapo wanajiamulia mambo yao wenyewe kaskazini mwa Irak- yaani jirani wa Uturuki. Kwa hiyo Kilichobakia kwa serikali ya nchi hiyo,ni kutumia mabavu kuwabana wakurdi wanaowakilishwa na chama cha PKK. Mhariri wa gazeti hilo anakumbusha uvamizi uliofanywa na majeshi ya Uturuki kusini mwa Irak.

Kwa kuwa chama hicho hakiwezi kukabiliana na serikali ya Uturuki kijeshi, kinatumia njia kama hizo za utekaji nyara ili kuihamasisha dunia juu ya tatizo la wakurdi nchini Uturiki.

Hatahivyo bado hakuna uhakika iwapo,ni PKK iliyowateka nyara watalii hao wa kijerumani.

Juu ya hayo gazeti la Badische Neueste Nachrichten linasema, ikiwa itathibitika kuwa ni PKK inayowashikilia wajerumani hao ,basi tukio hilo linaashiria mwanzo wa mgogoro wa hatari.
Lakini gazeti la Neue Westfällische linahoji kuwa kitendo hicho cha utekaji nyara kinaonesha jinsi chama cha PKK kilivyotamauka.

Juu ya mkutano wa viongozi wa nchi tajiri uliomalizika jana nchini Japan,

gazeti la Volkstimme linasema mambo yanaenda polepole lakini yanasonga mbele, na hasa kuhusu suala la hali ya hewa.

Hata ikiwa India na China pia zinabeba lawama juu ya kuchafuka kwa hali ya hewa, sawa na Marekani,yafaa kutambua kwamba dunia yote ni sawa na watu wanaosafiri katika mtumbwi mmoja.

Jee itakuwa sawa kwa Barack Obama kuhutubia mjini Berlin?

Mhariri wa gazeti la Mitteldeutsche anasema hapana. Obama ni mjumbe wa chama cha Demokratik aneawania urais nchini Marekani ,kwa hiyo haitakuwa sawa kwa Ujerumani kujiingiza katika kampeni yake. • Tarehe 10.07.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EZo1
 • Tarehe 10.07.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EZo1