Maoni ya wahariri juu ya sheria ya kupambana na ugaidi | Magazetini | DW | 18.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya sheria ya kupambana na ugaidi

Wahariri wanatoa maoni juu ya sheria ya kupambana na ugaidi iiyopitishwa nchini Misri.Baadhi wanahofia huenda sheria hiyo ikahujumu uhuru wa vyombo vya habari.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi

Mhariri wa gazeti la "Reutlinger - General Anzeiger anasema sheria ya kupambana na ugaidi iliyopitishwa nchini Misri kwa mara nyingne inaonyesha jinsi nchi za magharibi zilivyokuwa tayari kumvumilia dikteta madhali anahikisha usalama na utulivu wa nchi kama jinsi ilivyokuwa wakati wa Rais Mubarak.


Mhariri wa gazeti la "Brauschweiger" pia anasema sheria ya kupambana na ugaidi iliyopitishwa na Misri inaziweka nchi za magharibi katika hali ya kutatanisha.Mhariri huyo anaeleza kwamba wanasiasa wa nchi za magharibi wamelemewa kuhusu hali ya Mashariki ya Kati. Suala la kuhakikisha utulivu wa nchi ni muhimu kwa wanasiasa hao.

Wanapaswa kukumbuka yaliyotokea nchini Syria na Libya yaliyosababisha kuzuka na kustawi kwa magaidi wanaoitwa dola la kiislamu.Na sasa huenda wanasiasa wa nchi za magharibi wakayafunga macho yao yote katika kuzifurahia kandarasi za mfereji wa Suez.

Ujerumani na IMF zavutana juu ya Ugiriki

Gazeti la "Lausitzer Rundschau" linazungumzia juu ya mvutano baina ya Ujerumani na Shirika la fedha la Kimataifa,IMF kuhusu madeni ya Ugiriki.Mhariri wa gazeti hilo anasema sasa Shirika la Fedha la Kimataifa linataka Ugiriki ipunguziwe mzigo wake wa madeni. Lakini shirika la IMF linasema hayo likiwa linajua vizuri, kuwa kwanza lingetaka kulipwa fedha zake.

Gazeti hilo linasema kwa utaratibu huo mabilioni yaliyotolewa na walipa kodi wa Ujerumnai yangelipotea. Mhariri wa "Lausitzer Rundschau " anasema Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesisimama imara kuupinga mpango huo angalau mpaka mwaka wa 2017 utakapofanyika uchaguzi nchini Ujerumani.


Gazeti la "Lausitzer Rundschau" linalitilia maanani pendekezo la Kansela Merkel kwa shirika la fedha la kimataifa juu ya kuipa Ugiriki muda mrefu zaidi ili iweze kuyalipa madeni yake. Mhariri wa "Thüringer Allgemeine " anasema siyo waasi tu ,na Urusi, inayowaunga mkono wanaoyakiuka makubaliano ya kudumisha amani mashariki mwa Ukraine.

Serikali ya Ukraine pia inayakiuka makubaliano hayo.Sera ya vikwazo ya Ukraine, inayoungwa mkono na nchi za magharibi haijaleta tija kwa watu wa jimbo la Donbass mashariki mwa Ukraine. Pamoja na hayo rushwa inastawi nchini Ukraine na wapiganaji wa hiari hazifuati amri za makanda.Watu hao walipaswa kunyang'anywa silaha siku nyingi.

Mwandishi:Mtullya Abdu./deutsche Zeitungen .

Mhariri:Mtullya Abdu.