Mali asili muhimu kuingiza China katika teknolijia ya juu | Matukio ya Kisiasa | DW | 26.08.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mali asili muhimu kuingiza China katika teknolijia ya juu

Mali asili ya madini kama Yittrium, Prometheum ama Neodym inapatikana China na madini hayo yanayotumika katika uzalishaji wa vifaa vya teknolojia yataiingiza China katika nguvu kubwa duniani.

default

Moja ya kampuni zinazohamishia teknolojia yake nchini China ni kampuni ya Siemens ya Ujerumani .

Ni  majina  ya  watu  mashujaa   katika    ulimwengu  wa vichekesho. Yittrium , Prometheum  ama   Neodym.   Tatu kati  ya  jumla   ya   maliasili   hizo  17  zinafahamika   kama ardhi  takatifu.  Hali  yake   inafanya    madini  hayo   kuwa muhimu  sana   kwa  ajili  ya  viwanda  vya  teknolojia  ya juu. China  inadhibiti   sehemu  kubwa  ya   soko   la  dunia kwa  asilimia  95  na  kubana  mauzo  ya  nje.

Guo Yun  ni  mwanasayansi   katika  chuo  kikuu kilichoko   mashariki  ya   China  cha  sayansi  na teknolojia  mjini  Shanghai.  Eneo  lake  maalum  ni  kile kinachoitwa   ardhi  tukufu.

Wachina  wana thamini  sana  ardhi  yao  tukufu. Deng Xiaoping   ndie  aliyetoa  sentensi  hiyo  maafuru. Mashariki  ya  kati  wana  mafuta, sisi  tuna  ardhi  tukufu.

Wameweza   kwa  muda   wa  hivi  karibuni  kushughulika sana  katika  mali  asili, hususan   katika  eneo  la teknolojia  ya   juu. Kwa  mfano   madini  ya  Neodym . Yanatumika  katika   kuimarisha  sumaku  katika  vyuma. Yanaweza  kuimarisha   chuma   kupata  sumaku inayoweza  kubeba  uzito  mara  1300  zaidi.

Madini   hayo  yanaweza  kutumiwa  katika  maeneo mengi, iwapo   mtu  anahitaji  eneo  imara   la  sumaku kwa  matumizi  ya  sehemu  ndogo. Katika  vitambuzi  vya kompyuta   na  kasi   katika  matumizi  ya  kompyuta  ama pia   katika  vipaza  sauti  ama  spika  za  simu  za  mkononi zinazojulikana  kama  smart phones.

Karibu  nusu  ya  mahitaji  ya  dunia  ya  ardhi  tukufu  ama udongo  mtukufu yanatoka  Baotou, mji  wenye  watu milioni  mbili  katika  eneo  la  Mongolia. Hapa  kuna  mgodi wa  Bayan Obo, mgodi  mkubwa  kabisa  duniani   wa maliasili  hiyo  ya  udongo  mtukufu. Kwa  miaka  kadha China  imekuwa  ikijaza soko  la  dunia   kwa   maliasili  hiyo na   kuwabana  washindani  wake.  Hii  leo  China inadhibiti  soko  la  dunia. Duniani  kote  kiasi  cha  asilimia 95  ya  udongo  huo muhimu  unapatikana  kutoka  China. Sasa  nchi  hiyo   inataka  kubadilisha   jukumu  lake  la usafirishaji  wa  mali  hiyo  ya  asili. Udongo  huo  wa manufaa  utakuwa  ndio njia  ya  kuingia  katika  uzalishaji wa  vifaa  vya  teknolojia   duniani.  Kwa  mwanauchumi  Hu Xingdou   kutoka  chuo  kikuu  cha  sayansi  na  teknolojia cha  China  anasema  kuwa   udongo  huo  ni chombo muhimu  cha  mkakati  kwa  China.

Ni  dhahiri  kuwa  hilo  ni  jambo  zuri  kwa  China,  kwa kuwa  iwapo  una  maliasili  kama  hiyo, inakufanya  uwe na  chombo  cha  mkakati.  China  inaweza  kuamua  kuuza maliasili  hiyo  kwa  nchi  fulani  tu, ambazo  inazitaka, na kuzifungia  nyingine  kupata  mali  hiyo.

Pamoja  na   hali  hiyo  ya  kuziondoa  baadhi  ya  nchi kutoka  mauzo   ya  mali  hiyo  ya  asili  makampuni  ya teknolojia  ya  juu  kuhamia  China   ni  athari  ambayo China   ilikuwa  inamatamanio  nayo   makubwa. Pia kutokana  na   hali  isiyoweza  kuzuilika  ya  kuhamishia teknolojia   nchini  China.

Mwandishi:  Matthias  Hein / ZR /  Sekione  Kitojo

Mhariri : Josephat  Charo.

 • Tarehe 26.08.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OxEn
 • Tarehe 26.08.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OxEn
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com