1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Mali

Mali ni taifa lililozungukwa na nchi kavu magharibi mwa Afrika. Ni taifa la nane kwa ukubwa barani Afrika likiwa na ardhi yenye ukubwa wa kilomita za mraba 1,240,000. Lina wakaazi milioni 15.5 na mji mkuu wake ni Bamako.

Nchi ya sasa ya Mali ilikuwa sehemu ya himaya tatu za Afrika Magharibi zilizodhibiti biashara ya eneo la Sahara: Himaya ya Ghana, himaya ya Mali ambayo ndiyo chimbuko la sasa la jina la nchi hiyo, na himaya ya Songhai. Mali imekuwa ikikabiliwa na migogoro ya kivita tangu mwaka 2012 wakati wapiganaji wa kabila la Tuareg waliponazisha uasi kutaka kujitenga kwa eneola Mali ya kaskazini. Wapiganaji wa Kiislamu walitumia fursa hiyo kutaka kuunda taifa linalofuata sheria za Kiislamu kabla ya Ufaransa kuingilia kati na kuwafurusha.

Onesha makala zaidi