1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Utawala wa Mali wanuia kurejesha shughuli za kisiasa

11 Julai 2024

Utawala wa kijeshi wa Mali umetangaza jana Jumatano azma yake ya kuruhusu tena shughuli za kisiasa ilizozisimamisha mwezi Aprili.

https://p.dw.com/p/4i88L
Mali | Kanali Assimi Goita
Kiongozi wa serikali ya kijeshi nchini Mali Kanali Assimi Goita amesema ataruhusu kurejea kwa shughuli za kisiasa zilizozuiwa nchini humo tangu mwezi ApriliPicha: OUSMANE MAKAVELI/AFP/Getty Images

Taarifa ya baraza la mawaziri imesema serikali imeamua kuondoa kizuizi hicho dhidi ya vyama na taasisi za kisiasa.

Mkuu wa serikali ya kijeshi Kanali Assimi Goita alihalalisha hatua hiyo akiangazia kile alichotaja kama mijadala isiyo na maana ya vyama vya siasa pamoja na upotoshaji, ambayo alisema vilihatarisha "mazungumzo" yanayoendelea ya kitaifa kuhusu mustakabali wa kisiasa wa Mali.

Vyama hivyo wakati huo vilikuwa vinapinga uamuzi wa watawala wa kijeshi kusalia madarakani hadi baada ya mwezi Machi mwaka huu, ambao ndio ulikuwa ukomo wa muda wao wa kutawala.