Malengo ya milenia ya maendeleo:Mtazamo wa Ujerumani
20 Septemba 2010
Miundo iliyopo sasa katika nchi mbalimbali haitoshelezi katika
kufanikisha lengo la keleta mfumo thabiti wa utawala bora
duniani.Jee sasa pana matumaini gani?
Wizara ya Ujerumani ya maendeleo ya uchumi na ushirikiano iliwaalika wataalamu mjini Berlin kujadili utawala bora duniani kwa kuzingatia malengo ya maendeleo ya Millenia.
Mnamo kipindi cha miaka mitano ijayo, malengo ya maendeleo ya Millenia yanapaswa kufikiwa, kama jinsi nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walivyokubaliana miaka 10 iliyopita.Hatua fulani zimeshachukua hadi sasa katikaa juhudi za kuyatekelezamalengo hayo, yaani kuupunguza umasikini duniani kote kwa nusu, kutoa elimu ya msingi kwa watoto wote na kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake.
Malengo hayo yanapaswa kutekelezwa hadi kufikia mwaka wa 2015.
Lakini kadri tunavyousogelea mwaka huo ndivyo inayvozidi kudhihirika kwamba, ili mafanikio katika kuyafikia malengo hayo ya maendeleo ya Millenia,yanatangamana na muundo wa utekelezaji unaofanya kazi kwa ufanisi.Kinachohusika hapa ni matatizo ya dunia na kwa ajili hiyo panahitajika majawabu katika ngazi ya kidunia.Dirk Messner,mkurugenzi wa chuo cha Ujerumani cha sera za maendeleo amesema kuwa,''Tunachojadili sasa,ikiwa mtu anafikiria juu ya utawala wa dunia au ikiwa mtu anafikiria masuala ya msingi kama vile,hali ya hewa, chakula an nishati, mtu ataweza kubaini kwamba hapa anakabiliana na suala la mataifa kutegemeana.Mawazo ya zamani yalikuwa juu ya nchi kuwa huru kwa kadri ilivyowezekana ili iwajibike kwa wananchi wake.''
Shirika lisilokuwa na makali
Lakini sasa tunakabiliwa na mazingira ya kutegemeana yanayopaswa kujengwa katika msingi wa kisiasa.Hiyo ni changamoto iliyopo katikaa kuufikia utawala wa dunia.
Mashirika ya kimataifa yaliyopo sasa hayatoshi katika kuikabili changamoto hiyo.Mfano ni Umoja wa Mataifa wenye wanachama 189.Umoja wa Mataifa una uhalali wa kiwango cha juu, lakini panapotokea migogoro, Shirika hilo linakosa uwezo wa kupitisha maamuzi.
Au tuchukue mfano wa taasisi kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa,IMF. Ni kweli kwamba mashirika hayo yana uwezo wa kutekeleza maamuzi kwa njia ya ufanisi, lakini hayachukui wajibu wa kuiwakilisha jumuiya ya kimataifa.Hayo yanayahusu majopo yenye nguvu kama ya G7 au G8 ya nchi tajiri duniani.Hata hivyo sasa pana kundi la nchi 20. Juu ya jumuiya ya nchi hizo 20 mkurugenzi wa chuo cha Ujerumani cha sera za maendeleo Dirk Messner ameeleza,''Tunayo mapinduzi madogo ambayo wengi hawakuyaona.Tumeweza kuona mabadiliko, kutoka kwenye uchumi wa dunia uliokuwa unaoendeshwa na nchi za G 8 kwenda kwenye uchumi wa dunia unaondeshwa na nchi za G 20- yaani nchi zinazoinukia kiuchumi na nchi nyingine zinazoendelea."
Mkurugenzi huyo amesema kuwa huo ni mwelekeo mzuri, kwani nchi nyingi zinazoinukia na zinazoendelea, hapo awali hazikuwa na uwezekano wa kushiriki katika michakato ya maendeleo na ya kisiasa katika ngazi ya kimataifa.Mkurugeni Messner amaeeleza kuwa kwa njia hiyo sauti za nchi zinazoendelea zitaweza kusikika vizuri zaidi.
Mwandishi/ Mtulya Abdu-ZPR-Kiesel Heiner
Mpitiaji/....Mwadzaya,Thelma