1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makadirio ya kutia moyo ya ukuaji wa kiuchumi nchini Ujerumani

Oumilkher Hamidou21 Oktoba 2010

Uchumi wa Ujerumani unatazamiwa kukuwa kwa asili mia 3.4 kwaka huu,hali inayotarajiwa kuimarisha soko la ajira humu nchini

https://p.dw.com/p/PkCt
Waziri wa uchumi Rainer BrüderlePicha: dapd

Serikali kuu ya Ujerumani imerekebisha makadirio ya ukuaji wa kiuchumi kwa mwaka 2010 na kusema ukuaji huo wa kiuchumi utafikia asili mia 3.4.Waziri wa uchumi Rainer Brüderle wa kutoka chama cha kiliberali cha FDP ametangaza habari hizo hii leo mjini Berlin.Hapo awali serikali kuu ilikadiria ukuaji wa kiuchumi wa asili mia moja nukta nne kwa mwaka huu.Kwa mwaka 2011 serikali inategemea pato la ndani litaongezeka kwa asili mia moja nukta nane badala ya asili mia moja nukta sita zilizotangazwa hapo awali.

Angalao safari hii waziri huyo wa uchumi wa kutoka chama cha kiliberali alikuwa na kila sababu ya kuonyesha ameridhika,alipozungumza na waandishi wa habari.Alikua anatabasamu mwenyewe alipowatangazia waandishi habari makadirio mepya ya kiuchumi .

"Ukuaji wa kiuchumi ni bayana tena ni wa nguvu.Tunategemea ukuaji wa kiuchumi wa asili mia tatu nukta nne kwa mwaka huu.Ukuaji wa kiuchumi wa namna hii,umeshuhudiwa mara moja tuu tangu wimbi la neema ya muungano-mwaka 2006 tulikuwa pia na ukuaji wa kiuchumi wa asili mia tatu nukta nne.Ujerumani kwa hivyo inaongoza barani Ulaya linapohusika suala la hali nzuri kiuchumi- Ujerumani ni nchi ambayo uchumi wake unakuwa."

Ukuaji wa kiuchumi usiokua na mfano anasema waziri Brüderle uliochochewa na kutulia hali ya kiuchumi ulimwenguni na biashara ya nje -kiini kikikutikana katika bidhaa za viwandani na ufundi.Vitega uchumi vimeleta tija na hali katika soko la ajira na wafanyakazi itaimarika.

Kuanzia msimu huu wa mapukutiko idadi ya wasiokua na ajira inatazamiwa kupunguwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1992 na kusalia chini ya watu milioni tatu na mnamo mwaka 2011 idadi yao itazidi kupungua.

Hata hivyo mwakani serikali kuu ya Ujerumani inakadiria ukuaji wa kiuchumi utafikia asili mia moja nukta nane.

G20 Treffen Busan Südkorea
Mawaziri wa fedha wa G-20 walipokutana Busan Korea ya kusini mwezi June mwaka huu.Picha: AP

Katika mkutano wa mawaziri wa fedha wa kundi la mataifa yanayoendelea na yale yanayoinukia-G20 nchini Korea ya kusini,ambako waziri wa uchumi wa serikali kuu ya Ujerumani atamuwakilisha waziri wa fedha Wolfgang Schäuble ambae ni mgonjwa kwa sasa,bwana Rainer Brüderle anasema atapigania utaratibu wa ushirikiano na kujumuishwa China ili kuepusha kile kiitwacho "vita vya sarafu."

Katika mahojiano kabla ya kuondoka kuelekea Korea ya kusini,waziri Brüderle ameonya mvutano wa sarafu unaweza haraka kugeuka kuwa mvutano wa kibiashara.

Mwandishi:Gräßler Bern(DW Berlin)/Hamidou Oummilkheir

Mpitiaji:Josephat Charo