1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano yazidi Israel Netanyahu akifanya ziara Ujerumani

Zainab Aziz
16 Machi 2023

Maanamano yanaendelea nchini Israel wakati waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu anafanya ziara nchini Ujerumani. Watu wanaandamana kupinga mageuzi yenye utata ya mahakama

https://p.dw.com/p/4Omhl
Israel - Demo in Jerusalem
Picha: Saeed Qaq/imago images/ZUMA Wire

Maandamo hayo yanafanyika kwenye sehemu mbalimbali za mji wa pwani wa Tel Aviv. Waandamanji walipambana na polisi, baadhi yao walizuia njia inayoelekea kwenye mji wa Jerusalem.

Ziara ya Netanyahu yaitia kishindo Ujerumani

Maandamano mengine yamepangwa kufanyika leo wakati waandamanji wengine wamejikusanya mbele ya ubalozi wa Ujerumani mjini Tel Aviv.

Rais wa Israel Isaac Herzog amependekeza kuwepo mwafaka ili kuleta suluhisho la mgogoro huo. Hata hivyo, Netanyahu alilipinga pendekezo hilo kabla ya kuanza ziara ya nchini Ujerumani.