1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Serikali ya Uingereza yadai wanamaji wake kurejeshwa kutoka Ghuba ya Uajemi

23 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGB

Serikali ya Uingereza inadai kuachiwa huru na kurejeshwa salama kwa wananamaji wake 15 haraka iwezekanavyo .Wanamaji hao walikamatwa na majeshi ya wanamaji wa Iran walipoingia eneo la Iran kwenye Ghuba la Uajemi.Kisa hicho kilitokea hii leo.Wanajeshi hao walikuwa wakifanya ukaguzi wa kawaida kwenye meli ya biashara.Waziri wa Mambo ya kigeni wa uingereza Margaret Beckett anaitisha kikao na balozi wa Iran nchini humo.

Wakati huohuo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mabadiliko kidogo kwenye rasimu ya mapendekezo ya kuwekea vikwazo nchi ya Iran baada ya nchi hiyo kukataa kusitisha mpango wake ya kurutubisha madini ya uranium.Baraza hili linatarajiwa kupiga kura ya kuidhinisha vikwazo hivyo hapo kesho baada kufanya kikao cha siri jana jioni.Kulingana na Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa Emyr Jones Parry rasimu hiyo iko tayari kupigiwa kura na wanapanga mkutano wa mwisho hii leo.

Rasimu hiyo inalenga kupiga marufuku nchi ya Iran kutouza silaha katika mataifa ya nje vilevile kuwekewa vikwazo vya biashara.Aidha inaipa nchi ya Iran miezi miwili kutimiza masharti hayo au kuwekewa vikwazo vya kiuchumi bila vya kijeshi.Iran kwa upande wake inashikilia kuwa haibadili msimamo wake na ilianzisha mazoezi ya kijeshi kuonyesha nguvu zake za kujilinda.