LONDON:Fiji yaondolewa katika jumuiya ya madola kwa muda | Habari za Ulimwengu | DW | 09.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Fiji yaondolewa katika jumuiya ya madola kwa muda

Jumuiya ya madola imeiondoa kwa muda Fiji na kutangaza vikwazo kadhaa dhidi ya taifa hilo kufuatia mapinduzi ya kijeshi nchini humo.

Hayo yametangazwa hapo jana katika mkutano wa dharura wa mawaziri wa jumuiya hiyo mjini London.

Mawaziri hao pia wamesimamisha mipango yake ya usaidizi wa kiufundi kwa taifa hilo.

Kamanda wa kijeshi wa Fiji Commodore Frank Bainimarama aliyeongoza mapinduzi hayo ya kijeshi ambayo hayakusababisha umwagikaji wa damu alitangaza kuidhibiti nchi jumanne iliyopita.

Hii ni mara ya nne kwa taifa hilo kushudia mapinduzi na mara ya nne kuondolewa kwa muda kwenye jumuiya ya madola katika kipindi cha miongo miwili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com