LONDON: Uingereza yakumbuka mashambulizi ya Julai 7 2005 | Habari za Ulimwengu | DW | 07.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Uingereza yakumbuka mashambulizi ya Julai 7 2005

Uingereza hii leo inaadhimisha mwaka wa pili tangu kufanywa mashambulizi ya Julai 7 mwaka 2005 mjini London.Wakati wa majira ya joto ya mwaka 2005,Waingereza 4 wa Kiislamu waliojitolea muhanga walijiripua katika basi moja na treni tatu zinazokwenda chini kwa chini.Watu 52 waliuawa katika mashambulizi hayo.Nchini Uingereza,kiwango cha tahadhari dhidi ya ugaidi kimepandishwa tena,kufuatia mashambulizi yaliyoshindwa ya kutaka kuripua mabomu katika miji ya London na Glasgow.

Waziri Mkuu Gordon Brown amesema,itakuwa vigumu kwa umma,lakini anaamini kuwa kwanza kabisa watu wanachotaka ni kuwepo usalama wanapokwenda sehemu zilizojaa watu.

Brown,anataka ushirikiano zaidi kati ya jeshi, polisi,idara ya upelelezi ya Uingereza na za kimataifa,katika vita dhidi ya ugaidi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com