LONDON: Mwanya wazidi kati ya matajiri na masikini | Habari za Ulimwengu | DW | 29.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Mwanya wazidi kati ya matajiri na masikini

Askofu Mkuu Desmond Tutu wa Afrika ya Kusini aliepewa Tuzo ya Amani ya Nobel,ameonya kuwa mwanya kati ya matajiri na masikini nchini Afrika ya Kusini,unazidi kuwa mkubwa.Tutu akizungumza mjini London,alikosoa mwendo wa pole pole wa kugawa upya utajiri wa nchi, tangu serikali ya ubaguzi kuondoshwa hapo mwaka 1994.Hii si mara ya kwanza kwa Tutu kukosoa sera za uchumi za Afrika ya Kusini,akisema siasa hizo zimetajirisha wachache na si walio wengi.Wakati huo huo amesifu ustahmilifu wa umma.Amesema,baadhi kubwa ya watu waliokuwa wakiishi vibandani wakati wa utawala wa wazungu,hata hii leo wanaendelea kuishi katika hali hiyo hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com